Kipenzi - Babu na mjukuu, mchoro wa Georgios Jakobides (1890)

Babu kwa mjukuu wake ni hasa baba wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%.

Inakadiriwa kwamba miaka 30,000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mang'amuzi mbalimbali kuliko awali.

Pia babu anaweza kushika nafasi ya baba ikiwa huyo hayupo (k.mf. amekufa) na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama baba yupo, babu anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto.

Tanbihi


Makala hii inatumia vifaa kutoka kwenye ukurasa wa Wikipedia Babu, iliyotolewa chini ya Creative Commons Attribution-Share-Alike License 3.0.